IQNA

Jumuiya ya CFCM yalaani matamshi yanayoupinga Uislamu ya Naibu Katibu Mkuu wa chama cha taifa Ufaransa

17:00 - December 12, 2010
Habari ID: 2046795
Baraza la Waislamu wa Ufaransa (CFCM) limelaani matamshi yanayopiga vita Uislamu yaliyotolewa na Katibu Mkuu wa chama cha Harakati ya Taifa ya Ufaransa (FN) Jean-Marie Le Pen.
Shirika la habari la AFP limeripoti kuwa Muhammad Musawi Mwenyekiti wa Baraza la Waislamu wa Ufaransa ametoa taarifa akiyataja matamshi yaliyotolewa na kiongozi huyo wa ngazi za juu wa chama cha FN kuwa si ya kuwajibika na kwamba yanawachochea wananchi kufanya ghasia na unyanyasaji dhidi ya Waislamu.
Sehemu nyingine ya taarifa hiyo ya Baraza la Waislamu wa Ufaransa imeashiria juhudi zinazofanywa na wananchama wa baraza hilo kwa ajili ya kutatua matatizo yanayohusiana na misikiti na maeneo mengine ya ibada ya Kiislamu na kutangaza kuwa shughuli zote za Waislamu wa nchi hiyo zinafanyika kwa mujibu wa sheria za nchi.
Mussawi amesisitiza kuwa baraza la (CFCM) halitavumilia matamshi kama hayo yanayotolewa dhidi ya Uislamu na amewataka raia wote wanaotetea amani kupambana na fikra zinazozusha hitilafu na mifarano katika jamii.
Naibu Mwenyekiti wa chama cha FN cha Ufaransa Jean-Marie Le Pen alisema Ijumaa iliyopita kwamba utekelezaji wa swala za Waislamu mitaani ni sawa na uvamiaji unaofanyika bila ya kutumia silaha. 710928
captcha