Gazeti la Daily News la Bahrain limeandika kuwa kalenda hiyo ambayo imekuwa ikichapishwa tangu mwaka 1984, imechapisha pia athari 24 za sanaa ya Kiislamu zinazoakisi historia ya Kiislamu.
Kalenda hiyo ya mwaka 2011 mbali na kuchapisha athari za sanaa ya Kiislamu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, imejumuisha pia kazi za sanaa za nchi nyingine kama Uturuki, Iraq, India na nchi za kaskazini mwa Afrika.
Mkuu wa jumba la makumbusho la Baitul Qur’ani la Bahrain Samar al Kilani amesema kuwa majmui ya kazi za sanaa hiyo ya ulimwengu wa Kiislamu inajumuisha sanaa za nchi mbalimbali zilizotayarishwa kuanzia karne ya 9 hadi 20 Miladia.
Amesema kuwa kalenda hiyo imetayarishwa kwa lengo la kuarifisha sanaa ya Kiislamu na kuwaenzi wasanii Waislamu katika vipindi mbalimbali vya historian na vilevile kustawisha sekta ya utalii wa Kiislamu. 710217