IQNA

Kongamano la Amani, Umoja na Usawa katika Mtazamo wa Qur’ani

16:27 - December 13, 2010
Habari ID: 2047490
Kongamano la Amani, Umoja na Usawa katika Mtazamo wa Qur’ani Tukufu limefanyika katika mji wa Lucknow katika jimbo la Uttar Pradesh nchini India.
Kituo cha habari cha Two Circles kimeripoti kuwa kongamano hilo limesimamiwa na Taasisi ya al Qur’an ya mji wa Lucknow na kuhudhuriwa na wasomi na maulamaa wa Kiislamu wa India.
Mwanaharakati wa masuala ya kijamii wa India Laxmishankra Acharya alihutubia kongamano hilo na kusema kuwa Uislamu unatangza amani, umoja, ubinadamu na mshikamano wa kijamii na kwamba wale wasiojua maana ya aya za kitabu kitakatifu cha Qur’ani ndio wanaoipachika dini hiyo tuhuma chafu.
Laxmishankra Acharya ameashiria baadhi ya aya za Qur’ani tukufu na kusema kuwa Qur’ani inasema waziwazi kuwa Mwenyezi Mungu anawapenda watu wasiowakera na kuwaudhi wanadamu wenzao na kwamba mtu anayemuua mwanadamu bila ya dhambi yoyote ni mithili ya mtu aliyeua wanadamu wote na anayemwokoa mtu asiyekuwa na hatia huwa ameokoa na kunusu wanadamu wote.
Daktari wa Kiislamu wa India Jamiil Ahmad pia amehutubia kongamano hilo akisema kuwa idadi kubwa ya wanadamu duniani hawaelewi lengo lao maishani ilhani Qur’ani Tukufu imeainisha lengo la maisha ya mwanadamu ambalo iwapo litafuatiliwa litamdhaminia kiumbe huyo maisha ya saada na ufanisi. 711701
captcha