Jarida hilo linalochapishwa na Taasisi ya Kiutamaduni ya Quds katika mji wa Mash'had nchini Iran limejadili masuala muhimu katika ulimwengu wa Kiislamu, suala la kuyakurubisha madehehebu ya Kiislamu na vilevile kadhia ya Palestina na Quds Tukufu.
Katika makala maalumu jarida la Quds limeangazia kongamano la kukurubisha madhehebu ya Kiislamu lililowahi kufanyika Makkah. Aidha jarida hilo lina makala kuhusu pongezi za maulamaa wa Kiislamu wa Iraq kwa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kufuatia fatuwa yake ya kupiga marufuku kuvunjiwa heshima shakhsia wanaoheshimiwa na Masuni.
Jarida la Quds pia lina hotuba za Sayyid Hassan Nasrullah Katibu Mkuu wa harakati ya Hezbullah kuhusu njama zinazofanywa dhidi ya harakati hiyo ya mapambano.
Jarida la Kiarabu la Quds lina makala za kiutafiti za wasomi mbalimbali katika ulimwengu wa Kiislamu lengo kuu likiwa ni kuimarisha umoja wa umma wa Kiislamu na kuimarishwa nafasi na satua ya Waislamu duniani.
712186