Kwa mujibu wa tovuti ya donnetonavis, waandamanaji wamekusanyika katika sehemu iliyofanyika kikao hicho na kukemea vikali hatua ya makundi hayo ya kibaguzi mjini Paris. Wamepiga nara za kulaani kikao hicho wakisema kuwa wabaguzi hao ndio wanaopaswa kufukuzwa Ufaransa na sio Waislamu.
Waandaaji wa maandamano hayo ambayo yameandaliwa na makundi yanayopinga ubaguzi pamoja na vyama vya kisiasa vya mrengo wa kushoto vya Ufaransa wametawanyika kwa amani polisi wa kulinda usalama wakiwa wamesimama pembeni.
Kikao hicho cha chuki dhidi ya Uislamu kimeandaliwa na mrengo wa kulia wa Ufaransa na kuhudhuriwa na wawakilishi 300 wa makundi yanayopinga Uislamu barani Ulaya. 714612