IQNA

Thailand mwenyeji wa kikao cha kwanza cha kimataifa cha Utafiti wa Kiislamu

14:18 - December 20, 2010
Habari ID: 2050221
Kikao cha kwanza cha kimataifa cha utafiti wa Kiislamu kimepangwa kufanyika kesho tarehe 21 hadi Alkhamisi 23 Disemba huko Thailand katika Chuo Kikuu cha Mwana Mfalme Songkla
Tovuti ya MCOT imeripoti kuwa kikao hicho kimeandaliwa na Chuo cha Utafiti wa Kiislamu kinachofungamana na chuo kikuu kilichotajwa.
Kikao hicho kinafanyika katika kalibu ya nafasi ya utafiti wa Kiislamu katika jamii katika kipindi hiki cha utandawazi.
Chuo Kikuu cha al-Azhar cha Misri, Wakala wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Thailand TICA na Taasisi ya Uendeshaji wa Mikoa ya Kusini mwa Thailand ni miongoni mwa taasisi ambazo zimesaidia kuandaa kikao hicho.
Kikao hicho kinachowashirikisha wawakilishi 400 kutoka nchi tofauti za dunia kitafunguliwa na Abhisit Vejjajiva Waziri Mkuu wa Thailand.
Kuchunguzwa fursa za utafiti wa Kiislamu katika ulimwengu wa Kiislamu kwa ujumla na hasa nchini Thailand na vilevile uzoefu wa mashirika na wataalamu wa Kiislamu katika uwanja huo, kwa madhumuni ya kunyanyua viwango vya utafiti wa Kiislamu kwa lengo la kukabiliana na changamoto za utandawazi ni miongoni mwa mambo yatakayochunguzwa katika kikao hicho cha kimataifa. 714779
captcha