IQNA

Erdoğan apongezwa kwa kushiriki katika maombolezo ya Ashura

14:27 - December 20, 2010
Habari ID: 2050375
Maulamaa wa Kishia nchini Saudi Arabia wamempongeza Waziri Mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdoğan kwa kushiriki katika majlisi ya maombolezo ya Imam Hussein AS ya Siku ya Ashura yaliyofanyika mjini Istanbul Uturuki.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Jumuiya ya 'Khiri wa Islah' ya Saudi Arabia imetoa taarifa ikisema kuwa viongozi katika Ulimwengu wa Kiislamu wanapaswa kuiga hatua hiyo ya Erdoğan.
Jumuiya ya 'Khiri wa Islah' inayowakutanisha pamoja maulamaa wa Kishia wa Saudia Arabia imesistiza kuwa: "Waziri Mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdoğan mwaka jana na mwaka huu ameshiriki katika maombolezo ya Siku ya Ashura na kusema kilio chetu kilianza miaka 1370 iliyopita." Taarifa hiyo imesema hatua ya kihistoria ya Erdoğan inaashiria mfungamano na njia sahihi na ujumbe mkubwa wa Imam Hussein AS, jambo ambalo litapunguza uhasama.
Itakumbukwa kuwa Alkhamisi iliyopita Waziri Mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdoğan alishiriki katika maombolezo ya Siku ya Ashura mjini Istanbul na kusema maafa yaliyompata Imam Hussein AS huko Karbala yanapaswa kuwa chanzo cha Umoja wa Waislamu Mashia na Masuni. Alitoa wito kwa Mashia na Masuni kuweka kando tofauti zao na kuungana.
715304




captcha