IQNA

Maonyesho ya sanaa ya Kiislamu yafanyika Munich

18:04 - December 20, 2010
Habari ID: 2050535
Maonyesho ya kazi za sanaa ya kale na ya kisasa ya Kiislamu yanafanyika hivi sasa katika jumba la makumbusho la Haus der Kunst katika mji wa Munich nchini Ujerumani.
Kituo cha habari cha Islam Today kimeripoti kuwa mji huo wa Munich ulikuwa mwenyeji wa maonyesho ya kwanza na makubwa zaidi ya sanaa ya Kiislamu katika nchi za Magharibi. Katika maonyesho hayo ambayo yalipewa jina la Maonyesho ya Kazi Kubwa Zaidi za Sanaa ya Waislamu, athari 3600 za Kiislamu zilionyeshwa katika vyumba 80. kimeripoti kuwa albamu tatu za maonyesho hayo zingali zinatambuliwa kama marejeo yanayotumiwa na wanahistoria wa sanaa.
Zaidi ya watu laki moja walitembelea maonyesho hayo ambayo yalikuwa makubwa zaidi ya sanaa ya Kiislamu.
Hivi sasa na baada ya kupita miaka mia moja, athari 30 za kazi hizo pamoja na kazi nyingine za wasanii wa zama hizi wa Kiislamu zikiwemo sanaa za uchoraji, picha, uchongaji vinyago, mitindo ya mavazi, ufaji wa madini na kadhalika zinaonyeshwa katika maonesho ya Munich kwa lengo la kujenga husiano kati ya sanaa ya Kiislamu ya sasa na ya kale.
Maonyesho hayo yataendelea hadi tarehe 9 Januari mwakani. 715094

captcha