Kwa mujibu wa gazeti la Al Sharq, maonyesho hayo yalifunguliwa Desemba 18 kwa mnasaba wa Siku ya Kitaifa ya Qatar.
Hassan Abdullah al Abdullah Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kisayansi ya Qatar ameema: "Maonyesho haya yanafunguliwa kila siku kuanzia asubuhi hadi jioni kwa lengo la kuarifisha miujiza ya Qurani na Sunnah".
Maafisa wa ngazi za juu wa utamaduni na wataalamu wa Qurani Qatar walihudhuria sherehe za ufunguzi wa maonyesho hayo ya Qurani. Siku ya Kitaifa ya Qatar huadhimishwa kwa kuandaa hafla mbali mbali zikiwemo zile za kiutamaduni na kidini.
715347