IQNA

Nyumba ya Mwenyezi Mungu al Kaaba yaoshwa kwa manukato ya Kashan

14:02 - December 22, 2010
Habari ID: 2051754
Nyumba ya Mwenyezi Mungu al Kaaba jana tarehe 15 Muharram ilioshwa kwa maji ya Zamzam na manukato halisi kutoka mji wa Kashan nchini Iran.
Kituo cha habari cha Muhit kimeandika kuwa sherehe za kuoshwa al Kaaba zilihudhuriwa na kiongozi wa eneo la Makka Tukufu Khalid al Faisal bin Abdul Aziz, msimamizi wa masuala ya Masjidul Haram na Masjidun Nabii Saleh al Hasin na wanadiplomasia wa nchi za Kiislamu walioko nchini Saudi Arabia.
Katika sherehe hizo kuta za ndani ya al Kaaba zilioshwa kwa maji ya Zamzam na manukato kutoka Kashan.
Nyumba ya Mwenyezi Mungu al Kaaba huoshwa mara mbil kila mwaka, katikati ya mwezi wa Muharram na mwanzoni mwa mwezi mtukufu wa Ramadhani. Vilevile pazia la al Kaaba hubadilishwa mara moja kila mwaka mwanzoni mwa mwezi wa Dhil Hijja. 716088
captcha