Kwa mujibu wa gazeti la kieneo la Dar al-Hayaat, majmui ya vitabu hivyo vilivyochapishwa na taasisi ya Dar al-Amir ya Lebanon imechukua nafasi ya pili ya mauzo mengi ya vitabu vya kidini.
Kitabu cha Swiraat al-Mustaqeem cha Abdallah al-Harari kilichochapishwa na taasisi ya Dar a-Mashaari' ya Lebanon ndicho kitabu kilichochukua nafasi ya kwanza katika sekta hiyo ya mauzo ya vitabi vya kidini.
Duru ya 54 ya maonyesho hayo ya kimataifa ya vitabu yaliyoyashirikisha mashirika mbalimbali ya uandishi na uchapishaji vitabu ikiwemo Taasisi ya Fikra ya Kiislamu na Taasisi ya al-Huda ya Uchapishaji wa Kimataifa inayofungamana na Taasisi ya Utamaduni na Uhusiano wa Kiislamu ya Iran ilifanyika mjini Beirut tokea tarehe 6 hadi 16 Disemba. Zaidi ya mashirika 200 ya Lebanon, nchi za Kiarabu na kimataifa yalishiriki kwenye maonyesho hayo. 716849