Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, kikao hicho cha siku moja kimehudhuriwa na Hadi Azizzuddin Naibu Katibu Mkuu wa Shirika la Kiislamu la Sayansi, Utamaduni na Elimu ISESCO ambaye anamuwakilisha Dr. Abdulaziz Al-Tuwaijri Katibu Mkuu wa ISESCO. Kongamano hilo linafanyika katika makao makuu ya ISESCO mjini Rabat.
Wanachama wa Baraza la Ushauri Kuhusu Utekelezaji Mkakati wa Utamaduni katika Ulimwengu wa Kiislamu wamemchagua Bilal al Badur Naibu Waziri wa Utamaduni wa Imarati kuwa mwenyekiti mpya wa baraza hili.
Washiriki katika kikao hicho cha Rabat watajadili ajenda ya kikao kijacho cha saba cha mawaziri wa utamaduni wa nchi za Kiislamu kitakachofanyika mwakani katika mji wa Tlemcen nchini Algeria ambao umechaguliwa kuwa mji mkuu wa kiutamaduni katika ulimwengu wa Kiislamu mwaka 2011.
Kikao cha Kumi cha Baraza la Ushauri Kuhusu Utekelezaji Mkakati wa Utamaduni katika Ulimwengu wa Kiislamu kimetoa taarifa ya mwisho baada ya kumalizika na kusisitiza juu ya utekelezaji maamuzi yalichochukuliwa.
718105