IQNA

Mkutano wa kukurubisha madhehebu ya Kiislamu kufanyika Najaf

17:28 - December 28, 2010
Habari ID: 2055071
Mwenyekiti wa Baraza la Mkoa wa Najaf nchini Iraq ametoa wito wa kufanyika mkutano wa kimataifa wa kukurubisha pamoja madhehebu ya Kiislamu katika mji mtakatifu wa Najaf kwa ushirikiano wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu (OIC.
Faid Kadhim Nun ametoa wito huo katika mazungumzo yake na mwakilishi wa OIC nchini Iraq. Amesema kuwa historia ya mji mtakatifu wa Najaf inaambatana na elimu na maulamaa na kwamba mji huo una turathi nyingi za kale yakiwemo makaburi ya masahaba 700 wa Mtume na matabiina.
Kadhim Nun amesema katika kipindi cha uongozi wa Amirul Muuminin Ali bin Abi Twalib (as) mji wa Najaf ulikuwa mji mkuu wa dola la Kiislamu na hadi sasa mji huo unatoa mchango mkubwa katika masuala ya Kiarabu na Kiislamu hususan kadhia ya Palestina.
Mwenyekiti wa Baraza la Mkoa wa Najaf ameongeza kuwa mji huo uko tayari kikamilifu kwa ajili ya kuwa mwenyeji na mji mkuu wa kiutamaduni wa ulimwengu wa Kiislamu katika mwaka 2011 na kwamba serikali ya Iraq imetenga dola milioni 550 kwa ajili ya kutayarisha mji wa Najaf kama mji mkuu wa kiutamaduni wa ulimwengu wa Kiislamu.
Kwa upande wake mwakilishi wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC nchini Iraq Sadiq al Mahdi ameelezea kuridhishwa na kasi ya maandalizi ya mji wa Najaf kwa ajili ya kuwa mwenyeji wa mji mkuu wa kiutamaduni wa Kiislamu. Ameongeza kuwa OIC iko tayari kutoa msaada na uzoefu wake katika kufanikisha shughuli hiyo. 719811
captcha