IQNA

Mahafidh wa Qur'ani Tukufu waenziwa mjini Bensberg Ujerumani

13:07 - December 29, 2010
Habari ID: 2055448
Mahafidh kadhaa wa Qur'ani Tukufu wameenziwa katika sherehe maalumu iliyofanyika katika mji wa Bensberg nchini Ujerumani kwa udhamini wa sekretarieti ya Idara Kuu ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Sharja, moja ya Falme za Kiarabu zinazounda Imarati.
Mashindano ya hifdhi ya Qur'ani huandaliwa kila mwaka na idara kuu hiyo katika vituo vya Kiislamu katika nchi tofauti kwa lengo la kuwafikishia walimwengu ujumbe sahihi wa Kiislamu na kusahihisha fikra potofu iliyoenezwa ulimwenguni na maadui wa Kiislamu, kwa kutegemea thamani muhimu za mafundisho ya Kiislamu.
Sherehe hiyo imefanyika sambamba na kuandaliwa kwa kikao cha kila mwaka cha Baraza la Kiidara la Kituo cha Kiislamu na Kiutamaduni la Bensberg.
Viongozi wa kieneo na kimataifa wakiwemo meya wa Munich, balozi mdogo wa Marekani katika mji wa Bayern, Waziri wa Sheria wa Ujerumani, Mkuu wa chama cha Demokrasia ya Kijamii cha Ujerumani na Askofu mkuu wa Bayern wameshiriki katika kikao hicho kilichoandaliwa kwa shabaha ya kuuarifisha zaidi Uislamu katika eneo hilo. 720295
captcha