Mkuu wa Masuala ya Utamaduni katika Vyuo Vikuu vya Kidini Mkoani Khorassan Hujjatul Islam Muhammad Ramadhani amemwambia mwandishi wa IQNA kuwa kikao hicho kutahudhuriwa na Ayatullah Ayazi mwanazuoni mwandamizi katika Vyuo Vikuu vya Kidini vya Khorassan. Atatoa hotuba kuhusu maadili katika maisha ya Mtume SAW.
Kikao hicho kimeandaliwa kwa ajili ya wanachuo wa kike kutoka vyuo vya kidini vya Esmatia, Bibi Khadija na Bibi Zahra katika mkoa huo.
Idara ya Utamaduni katika vyuo vya kidini vya Khorassan imekuwa ikiandaa semina za mara kwa mara kuhusu sira ya Mtume SAW tokea mwanzo wa mwaka huu.
720068