IQNA

Maonyesho ya “Turathi ya Qur’ani, Ujumbe wa Amani” kufanyika California

14:34 - December 29, 2010
Habari ID: 2055661
Maonyesho ya “Turathi ya Qur’ani, Ujumbe wa Amani” yamepangwa kufanyika katika miezi ya mwanzoni mwa mwaka ujao katika Kituo cha Utamaduni wa Kiislamu katika mji wa Oakland Jimboni California Kaskazini.
Kituo cha Utamaduni wa Kiislamu cha California kitakachosimamia maonyesho hayo kimewataka Waislamu kuwasilisha athari zao za kisanii katika maonyesho hayo.
Kazi za kisanii za Kiislamu za makundi mawili ya watoto wenye umri wa kati ya miaka 5 hadi 14 na watu wenye umri wa zaidi ya miaka 15 katika sanaa za uchoraji, kaligrafia, upigaji picha na fani ya hati zinazohusu maudhui ya Qur’ani Tukufu zitaonyeshwa katika maonyesho hayo.
Wasanii watakaowasilisha kazi zao katika maonyesho hayo watazawadiwa loho za fahari.
Kituo cha Utamaduni wa Kiislamu cha California Kaskazini (ICCNC) ni shirika lisilokuwa la serikali ambalo linajishughulisha na kuarifisha Uislamu kupitia kazi za sanaa, utamaduni na ratiba mbalimbali za masomo. Kituo hicho pia kimekuwa kikitoa huduma mbalimbali kwa Waislamu na wasiokuwa Waislamu. 720693
captcha