IQNA

Spika wa zamani wa Bunge la Iran aandika Tarjumi ya Qur'ani

12:46 - December 30, 2010
Habari ID: 2055915
Tarjumi ya lugha ya Kifarsi ya Qur'ani Tukufu iliyoandikwa na Spika wa Zamani wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) Dkt. Gholam Ali Haddad Adel itachapishwa Machi mwaka 2011.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA Dakta Haddad Adel alianza kuiandika tafsiri hiyo miaka saba iliyopita na sasa iko katika hatua za mwisho kabla ya kuchapishwa. Katika tarjumi yake hiyo Haddad Adel amejitahidi kutumia lugha rahisi ili watu wote waweze kuifahamu Qur'ani Tukufu.
Kujitahidi kuwa karibu zaidi na lugha asili ya Qur'ani ni moja kati ya nukta muhimu za tarjumi ya Haddad Adel. Wasomi na wataalamu 100 wa sayansi za Qur'ani na fasihi wametoa maelekezo wakati wa kuandikwa tarjumi hiyo.
Haddad Adeli alianza kuandika tarjumi hiiyo ya Qur'ani kwa Kifarsi mwaka 1382 Hijria Qamariya (2003) wakati alipokuwa Mkuu wa Akademia ya Lugha na Fasihi ya Kifarsi.
719985
captcha