Shirika la habari la Kuwait (KUNA) limeripoti kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Uhispania Miguel Angel Moratinos amesema katika taarifa hiyo kwamba Quds ya Mashariki ni sehemu ya ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina na kwa mujibu wa sheria za kimataifa ni marufuku kujenga katika ardhi hizo.
Moratinos amesema uamuzi wa kuharibiwa jingo hilo umechukuliwa kwa lengo la kutayarisha uwanja wa kuendeleza ujenzi haramu wa vitongoji vya walowezi w Kiyahudi katika Quds Tukufu.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa pia ametoa taarifa akilaani vikali hatua hiyo ya Israel na akasema Israel inaendeleza siasa za kuharibu nyumba za Wapalestina na kughusubu mali na milki zao katika Quds Mashariki na inawafukuza Wapalestina katika nchi yao kinyume cha sheria na kuwaweka Wayahudi katika maeneo hayo.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa imetangaza kuwa kujenga katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina likiwemo eneo la Quds Mashariki, ni kikwazo cha juhudi za kurejesha amani katika Mashariki ya Kati na Israel inapaswa kuacha vitendo hivyo vya kichochezi. 728819