Hayo yamesemwa na Naib Caralic msomaji Qur'ani ambaye ameiwakilisha nchi yake ya Bosnia katika duru ya tatu ya mashindano ya kimataifa ya Qur'ani kwa wanachuo wa Kiislamu mjini Mash'had Iran.
Akizungumza katika mahojiana na shirika la habari za Qur'ani IQNA Caralich amesema kuwa yeye mwenyewe hujaribu kadiri anavyoweza kutekeleza katika maisha yake ya kila siku kila jambo analosoma katika kitabu hicho kitakatifu. Amesema kuwa njia bora zaidi ya kukabiliana na watu wanaoendesha uadui dhidi ya Uislamu duniani ni kuimarisha umoja na mshikamano wa Waislamu. Ameendelea kusema kuwa mifarakano na hitilafu miongoni mwa Waislamu ni mambo hatari yanayodhoofisha nchi za Kiislamu na kusisitiza kwamba maadamu sisi sote ni Waislamu tunapasa kufuata kikamilifu mafundisho ya Qur'ani Tukufu.
Caralic ambaye ni mwanachuo anayesoma masomo ya Kiislamu katika Chuo Kikuu cha Sarajevo amewashukuru waandaaji wa mashindano ya kimataifa ya Mash'had na kusema kuwa mashindano hayo yamefanikiwa kutokana na kutumiwa marefa waadilifu na wenye uzoefu mkubwa kuhusiana na masuala ya Qur'ani.
Amewataka wasomaji Qur'ani wa Iran watumwe nchini Bosnia Herzegovina ili kufanikisha zaidi shughuli za usomaji Qur'ani katika nchi hiyo ya Kiislamu barani Ulaya.
Caralic alikuwa mshindi wa pili katika duru ya 13 ya mashindano ya kimataifa ya usomaji Qur'ani yaliyofanyika mjini Zagreb, mji mkuu wa Croatia. 728154