IQNA

Ahmadinejad: Uhusiano wa kieneo utafaidisha ulimwengu wa Kiislamu

13:27 - January 15, 2011
Habari ID: 2064565
Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kuimarishwa ushirikiano kati ya nchi za eneo la Mashariki ya Kati ni kwa maslahi ya wananchi wa eneo hilo na ulimwengu mzima wa Kiislamu.
Akizungumza kwa nyakati tofauti kwa njia ya simu na Rais Abdullah Gul wa Uturuki na Sultan Qaboos bin Said al Busaidi wa Oman, Rais Ahmadinejad amesisitiza juu ya kuimarishwa mashirikiano kati ya nchi za eneo hilo na kuongeza kuwa, kuimarishwa mashirikiano hayo kutadhamini kupatikana amani na uthabiti.
Rais Gul na Sultan Qaboos wamesisitiza kwenye mazungumzo yao na Rais Ahmadinejad juu ya kuzidishwa kiwango cha mashirikiano kwa maslahi ya nchi za eneo na ulimwengu wa Kiislamu kwa ujumla.
Wakati huo huo Rais Ahmadinejad amempigia simu Mfalme Abdullah bin Abdul al-Aziz wa Saudi Arabia akimuombea dua ya kupona haraka.
Katika mazungumuzo hayo Rais Ahmadinejad alisisitiza kuwa ushirikiano wa nchi za eneo unaweza kuimarisha usalama Mashariki ya Kati.
Kwa upande wake Mfalme Abdullah wa Saudi Arabia amemshukuru Rais Ahmadinejad kwa kumjulia hali. Ameitakia taufiki serikali na taifa la Iran.
Mfalme Abdullah wa Saudi Arabia alikwenda mjini New York Marekani Novemba 22 kwa ajili ya matibabu.
730048

captcha