IQNA

Wairaqi wakaribisha programu za kumputa za Qur'ani kutoka Iran

12:54 - January 20, 2011
Habari ID: 2067822
Mwakilishi wa Taasisi ya Noor ya Iran nchini Iraq amesema kuwa wanafunzi wa vyuo vikuu, vyuo vya kidini na wasomi wa Iraq wamepokea vyema programu za komputa na bidhaa zinazotengenezwa na taasisi hiyo.
Sayyid Anwar al Husseini amesema kuwa kutokana na maendeleo ya teknolojia nchini Iraq na kustawi sekta ya teknolojia ya mawasiliano idadi ya watumiaji wa programu za komputa inaongezeka zaidi.
Sayyid Anwar al Hussaini ambaye ni mkurugenzi wa taasisi ya kusambaza vitabu ya Darul Nashr al Hussaini mjini Karbala amesema kwa sasa kuna idadi kubwa ya wahakiki wa vyuo vikuu vya kidini (hauza) na wasomi wanaotumia programu za komputa za sayansi ya Qur'ani, tafsiri, fiqhi na irfani.
Katika sehemu nyingine ya matamshi yake al Hussaini ameashiria maonyesho mbalimbali yanayofanyika nchini Iraq na akasema maonyesho hayo yanajumuisha pia programu za komputa za sayansi za Kiislamu na sayansi za jamii. 733403

captcha