Kwa mujibu wa gazeti la as-Sharq linalochapishwa nchini Qatar ratiba hizo za masomo zitawashirikisha wanawake, wanachuo wa kike, mabinti na vijana wadogo wa kike walio na umri tofauti. Masomo ya hifdhi kwa mabinti wa umri wa kati ya miaka minne hadi sita mashuhuri kwa jina la Zuhur al-Akhira yatakuwa yakifanyika siku za Jumanne na Jumatano za kila wiki.
Wazazi wa mabinti walio na umri huo mdogo wamefurahia sana masomo hayo na wamekuwa wakiwaandikisha kwa wingi watoto wao kwenye masomo hayo. Vilevile masomo mengine yaliyopewa jina la Manabir Min Nur maalumu kwa mabinti wenye umri wa miaka 9 hadi 11 yamepangwa kufanyika siku za Jumatatu na Jumatano.
Taasisi ya Sheikh Id imetangaza kuwa lengo la kufanyika masomo hayo ni kuwashawishi mabinti na wanawake wa Qatar kusoma na kuhifadhi Qur'ani Tukufu na pia kuwafanya wazingatie mafundisho ya kitabu hicho kitakatifu.
Taasisi hiyo kila mwaka huandaa masomo mengi ya Qur'ani kwa madhumuni ya kueneza utamaduni wa Qur'ani na Kiislamu katika jamii ya Qatar. 736948