IQNA

Tasisi ya mafunzo ya Qur'ani na kidini kuanzishwa Yemen

12:46 - February 10, 2011
Habari ID: 2078710
Taasisi ya mafunzo ya Qur'ani na kidini itazinduliwa hivi karibuni katika eneo la as-Swadiq katika mkoa wa Lahaj nchini Yemen.
Sherehe ya kuanza ujenzi wa taasisi hiyo ilifanyika Jumanne iliyopita kwa kuhudhuriwa na Abdul Qadir Ali Nassir mwakilishi wa gavana wa mkoa huo. Akizungumza katika sherehe hiyo, Ali Nassir amebainisha furaha yake kuhusiana na jambo hilo na kusema kuwa litasaidia pakubwa katika kuhudumia Qur'ani na jamii nzima ya Yemen. Ameelezea matumaini yake kwamba vijana watakaosoma masomo ya Qur'ani na kidini katika taasisi hiyo watahitimu na kuchukua nafasi muhimu za kuihudumia jamii ya Yemen katika siku zijazo.
Kwa upande wake Swadiq al-Makhlani, msimamizi wa taasisi hiyo amesema kuwa Wayemen wote walio na hamu ya kujifunza masomo hayo wataruhusiwa kufanya hivyo bila kizuizi chochote.
Ujenzi wa taasisi hiyo umekadiriwa kugharimu riali milioni 80 za Yemen. 745116
captcha