IQNA

Mustakbali wa uwekezaji wa Kiislamu wachunguzwa Bahrain

12:40 - February 12, 2011
Habari ID: 2079208
Mustakbali wa biashara na uwekezaji wa Kiislamu umechanguzwa katika kikao kilichofanyika hivi karibuni katika hoteli ya Crowne Plaza nchini Bahrain ambapo wakuu wa benki na mashirika ya kifedha pamoja na wataalamu wa masuala ya kiuchumi wameshiriki.
Kwa mujibu wa tovuti ya tradearabia.com kikao hicho kilichoandaliwa na Jumuiya ya Kimataifa ya Uchumi wa Kiislamu kilihudhuriwa pia na balozi wa Malaysia nchini Bahrain Bwana Sayyid Sultan Idris.
Jamil al-Jarudi, Mkurugenzi Mwandamizi wa Benki ya Elaf ambaye alikuwa mgeni wa heshima amezungumzia mustakbali wa biashara na uchumi wa Kiislamu na pia changamoto zinazoukabili. Vilevile wataalamu wa masuala ya kiuchumi walioshiriki kwenye kikao hicho wamechunguza suala hilo kwa kina.
Njadala kuhusu uoni mpana wa biashara na uwekezaji wa Kiislamu katika dunia ya leo ni lengo kuu la kufanyika kikao hicho. 745346
captcha