Katibu Mkuu wa Taasisi ya Kimataifa ya Kukurubisha Pamoja Madhehebu ya Kiislamu Ayatullah Muhammad Ali Taskhiri amesema kuwa kongamano hilo la Umoja wa Kiislamu litakalofanyika mjini Tehran litaangazia pia mikakati ya kuimarisha ukuruba wa madhehebu ya Kiislamu.
Akihutubia kikao cha waandishi habari Februari 13, Ayatullah Taskhiri ameashiria matukio ya kihistoria katika nchi kadhaa za Kiarabu na kusema kuwa kongamano lijalo la umoja wa Kiislamu litaangazia kwa kiwango kikubwa matukio hayo.
Aidha amesema kongamano la mwaka huu litatathmini makongamano 20 yaliyopita ya Umoja wa Kiislamu.
Kati ya watakaohudhuria kongamano hilo ni Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran atakayehutubu katika kikao cha ufunguzi na Dkt. Sayyed Mohammad Husseini Waziri wa Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu.
746919