IQNA

Wapalestina watatu wauawa shahidi na Wazayuni katika Ukanda wa Gaza

16:01 - February 19, 2011
Habari ID: 2083257
Raia watatu wa Kipalestina wameuawa shahidi katika mashambulio ya Wazayuni katika Ukanda wa Gaza.
Kwa mujibu wa gazeti la Arab News, siku ya Akhamisi alfajiri vifaru vya utawala ghasibu wa Israel vilivamia kambi ya wakimbizi ya Beit Lahya katika ukanda huo na kuwaua shahidi wavuvi watatu wa Kipalestina. Helikopta kadhaa za utawala huo pia zilishiriki katika shambulio hilo.
Siku ya Jumamtano iliyopita pia Wapalestina wawili walijeruhiwa katika shambulio kama hilo.
Ukanda wa Gaza unazingirwa na utawala haramu wa Kizayuni tokea mwaka 2006 kufuatia ushindi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas katika uchaguzi mkuu wa Palestina.
Tokea wakati huo hadi sasa Wapalestina wa Ukanda wa Gaza wamekuwa wakishambuliwa mara kwa mara na jeshi la utawala wa Tel Aviv, mashambulio makali zaidi yakiwa ni yale ya siku 23 yaliyoanza mwishoni mwa mwaka 2008. 749815
captcha