IQNA

Tafsiri ya kwanza ya Qur'ani kwa Braille

9:35 - February 26, 2011
Habari ID: 2086092
Tafsiri ya Kiingereza ya Qur'ani Tukufu iliyoandikwa kwa Braille (maandishi makhsusi kwa ajili ya vipofu) imechapishwa kwa mara ya kwanza na mtafiti na mtaalamu wa Qur'ani nchini Uturuki.
Kwa mujibu wa tovuti ya Moheet, Najmudin Uzun Oghlu, msomi wa Uturuki katika vyuo vikuu vya Marekani ametayarisha tafsiri hiyo ili kutatua matatizo ya wanafunzi vipofu ambao wanataka kusoma tarjumi ya Kiingereza ya Qur'ani.
Qur'ani hiyo inajumuisha jildi nane zenye kurasa 2000 na ilitayarishwa kwa muda wa miezi saba kwa ushirikiano na Waturuki na Wamarekani wenye ulemavu wa macho.
Mtafiti huyo kutoka Uturuki ambaye anazungumza lugha 9 anapanga kutayarisha tarjumai zingine za Qur'ani za Braille.
753262
captcha