
Uamuzi wa kuongeza muda huo ulikuwa na lengo la kutoa fursa pana kwa wapenzi wa Kitabu Kitukufu cha Allah kuweza kushiriki katika hafla hii ya kiroho.
Kwa mujibu wa Hujjatul-Islam Seyyid Nassereddin Nourizadeh, Mkuu wa Kituo cha Masuala ya Qur’ani chini ya Shirika la Wakfu na Misaada, licha ya kuwepo kwa changamoto za “vita vya tatu vilivyolazimishwa” (uchokozi wa Marekani na utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran), kumekuwa na ongezeko la idadi ya washiriki ikilinganishwa na duru zilizopita. Jumla ya watu 67,843 wamejisajili ili kuchuana katika kuwania nafasi za juu kwenye mashindano ya mwaka huu.
Baada ya mashindano hayo kufanyika katika ngazi za miji na mikoa, hatua ya fainali itafanyika kwa kuwakutanisha washindi wa ngazi za awali katika mji wa Zahedan, makao makuu ya mkoa wa Sistan na Balouchestan.
Mashindano haya ya Kitaifa ya Qur’ani Tukufu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, yanayoandaliwa na Shirika la Wakfu na Misaada, ndilo tukio kubwa zaidi la Qur’ani nchini humo, likiunganisha washiriki kutoka kila pembe ya nchi katika nyanja mbalimbali.
Mashindano haya ya kila mwaka, yanayotambulika kama tukio lenye heshima kubwa zaidi la Qur’ani nchini Iran, yana malengo ya kukuza thamani za Kiislamu, kuimarisha elimu ya Qur’ani, na kuibua vipaji adimu vinavyohudumia Kitabu cha Allah.
Mashindano hayo yanajumuisha vipengele mbalimbali, ikiwemo usomaji wa Qur’ani (Qiraa), Tarteel, hifdhi (kuhifadhi Qur’ani), na Adhana. Washindi wa kwanza watapata fursa ya kuiwakilisha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika mashindano ya kimataifa ya Qur’ani kote duniani, Insha’Allah.
4354438