IQNA

Warsha ya ‘Afya kwa Mtazamo wa Qur'ani’ kufanyika Iran

11:13 - February 28, 2011
Habari ID: 2087478
Warsha ya kwanza ya kitaifa yenye anwani ya ‘Afya kwa Mtazamo wa Qur'ani’ itafanyika kuanzia Machi 2-3 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Razi mjini Tehran.
Warsha hiyo imeandaliwa na Chuo Kikuu cha Sayansi za Tiba cha Tehran kwa ushirikiano na Chuo Kikuu cha Sayansi za Tiba cha Iran. Mada kuu katika warsha hiyo itahusu masuala ya kiafya katika Qur'ani Tukufu sura al Kahf.
Kuwasilisha maana ya afya kwa katika Qur'ani kwa mtazamo wa kisaikolojia, kifisiolojia, kijamii na kimaanawi katika maisha ya mwanadamu ni mada kuu zitakazojadiliwa kati ya wataalamu watakaoshiriki kikao hicho.
Madaktari na wataalamu watakaoshiriki katika warsha hiyo watatunukiwa shahada za ushiriki.
753949
captcha