IQNA

Tafsiri ya Qur'ani kwa lugha ya ishara yazinduliwa Jordan

11:07 - February 28, 2011
Habari ID: 2087479
Programu ya komyuta yenye tafsiri ya Qur'ani kwa lugha ya ishara imezinduliwa katika Kituo cha Kuhifadhi Qur'ani cha Jordan katika hafla iliyofanyika Februari 26.
Kwa mujibu wa gazeti la Al Ray, tafsiri hiyo ya Qur'ani inajumuisha mitazamo ya mufasirina kama vile Ibn Kathir, Montakhab, Tabari, Nasafi na al Muyassar.
Naibu Mkuu wa Kituo cha Kuhifadhisha Qur'ani cha Jordan Mohammad Khazar al Majali amesema mradi huo umekamilika baada ya juhudi za miaka mitano kwa wenye matatizo ya kusikia.
Amesema mradi huo ulianza baada ya kuchapishwa msahafu kwa Braille kwa ajili ya wenye ulemavu wa macho. Amesema tafsiri hiyo imetayarishwa kwa ushirikiano na Taasisi ya Kimataifa ya Ufuq.
754597

captcha