IQNA

Ayatullah Aarafi alaani mauaji ya kutisha Sudan, atoa wito hatua kuchukuliwa

18:58 - November 07, 2025
Habari ID: 3481480
IQNA-Ayatullah Alireza Aarafi, Mkurugenzi wa Vyuo Vikuu vya Kiislamu (Hauzah) nchini Iran ametoa ujumbe mzito wa kulaani mauaji ya kikatili dhidi ya watu wanyonge wa Sudan, akiwataka Waislamu na taasisi za kimataifa kuchukua msimamo wa wazi na wa dhati kuwasaidia Wasudan wanaodhulumiwa

 

Bismillahi Rahmani Rahim

"Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye tutarejea."

Katika nyakati hizi ambapo Umma wa Kiislamu unahitaji mshikamano, huruma, na kurejea katika misingi ya kibinadamu na ya  Mwenyezi Mungu, habari za mauaji ya kikatili dhidi ya watu wa Sudan zimeumiza nyoyo za kila mtu mwenye dhamira huru.

Janga hili la damu, lililotekelezwa kwa msaada wa moja kwa moja wa Uzayuni wa kimataifa na na madola ya kibeberu duniani pamoja na ushirikiano wa baadhi ya tawala za Kiarabu kutoka eneo la Ghuba ya Uajemi, ni mfano wa wazi wa njama za maadui wa Umma wa Kiislamu, njama za kueneza mgawanyiko, kupora rasilimali za mataifa, na kudhoofisha harakati za mwamko wa Kiislamu.

Hauzah za Kiirani na maulamaa wa Kiislamu, kwa msimamo thabiti, wamelaani jinai hii ya kutisha. Wanatoa wito kwa mataifa ya Kiislamu na wasomi wa ulimwengu wa Kiislamu kutokaa kimya mbele ya maafa kama haya, bali watetee misingi ya uhuru, heshima, na haki kwa kufichua mikono michafu ya madola ya kibeberu na vibaraka wao wa kikanda.

Ni wazi kuwa historia haitasamehe usaliti na ukimya mbele ya dhulma. Damu safi ya watu wa Sudan waliodhulumiwa, kama ilivyo damu ya mashahidi wa Gaza, Yemen, na Palestina, itazaa matunda ya mwamko na upinzani katika ulimwengu mzima wa Kiislamu.

Taasisi za kimataifa, Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC), na mashirika ya haki za binadamu yanatarajiwa kuchukua msimamo wa wazi na wa dhati dhidi ya janga hili la kibinadamu, badala ya kukaa kimya na kushindwa kuchukua hatua.

Hatimaye, tunatoa rambirambi na mshikamano wetu kwa familia zilizopoteza wapendwa wao na kwa watu wa Sudan waliodhulumiwa. Tunamuomba Mwenyezi Mungu awape subira, msaada, na ushindi, na alilinde Umma wa Kiislamu dhidi ya fitna na ubeberu wa madola ya kibeberu.”

Mauaji ya Kutisha ya RSF Yatikisa Sudan

Kikundi cha wanamgambo cha Rapid Support Forces (RSF), kinachoungwa mkono na utawala wa Kizayuni wa Israeli pamoja na Umoja wa Falme za Kiarabu ,(UAE) kimetekeleza uhalifu wa kutisha dhidi ya raia wa Sudan.

Wiki iliyopita, RSF waliteka mji wa El Fasher—ngome ya mwisho ya jeshi la Sudan katika eneo la Darfur—wakifanya mauaji na kuwakamata maelfu ya watu. Ripoti zinaeleza kuwa zaidi ya watu 2,000 waliuawa wakati wa uvamizi huo, huku mashuhuda wakidai kuwa idadi halisi ya waliopoteza maisha ni kubwa zaidi.

Picha za setilaiti zilizotazamwa na Maabara ya Utafiti wa Kibinadamu ya Chuo Kikuu cha Yale (HRL), pamoja na ushuhuda wa manusura, zinaonyesha mauaji ya halaiki barabarani na katika maeneo ya makazi, huku raia wakilengwa wakiwa wanajaribu kukimbia kuokoa maisha yao.

3495284

Kishikizo: sudan
captcha