Kongamano hilo la siku mbili limeandaliwa na Chuo Kikuu cha Sayansi za Tiba cha Tehran kwa ushirikiano na Chuo Kikuu cha Sayansi za Tiba cha Iran. Mada kuu katika warsha hiyo itahusu masuala ya kiafya katika Qur'ani Tukufu sura al Kahf.
Hafla ya ufunguzi imehutibiwa na Mahdi Feiz Mkuu wa Masuala ya Kiutamaduni katika Shirika la Jihadi ya Vyuo Vikuu Iran. Amesema mwaka huu kongamano la mwaka huu linajadili sura al Kahf na kwamba katika miaka ijayo sura nyingine za Qur'ani kuhusu afya zitajadiliwa na wasomi. Amongeza kuwa kwa mtazamo wa Qur'ani afya kamili inaweza kupatikana tu kupitia tauhidi.
Naye Sayyed Abul Hassan Shahzadeh Fazli Mkuu wa Kongamano hilo amesema kuna haja ya kubuniwa kituo maalumu kuhusu tiba ya Kiislamu.
Ali Muntadhari Mkuu wa Kituo cha Utafiti wa Tiba katika Shirika la Jihadi ya Vyuo Vikuu Iran amesema dhikri ya kumkumbuka Mwenyezi Mungu ni chanzo cha afya ya kisaikolojia.
Kuwasilisha maana ya afya katika Qur'ani kwa mtazamo wa kisaikolojia, kifisiolojia, kijamii na kimaanawi katika maisha ya mwanadamu ni mada kuu zitakazojadiliwa kati ya wataalamu watakaoshiriki kikao hicho.
Madaktari na wataalamu watakaoshiriki katika warsha hiyo watatunukiwa shahada za ushiriki.
756791