IQNA

Wizara ya Masuala ya Kidini ya Palestina yalaani kubomolewa maeneo ya Msikiti wa al-Aqsa

18:29 - March 06, 2011
Habari ID: 2091229
Wizara ya Masuala ya Kidini ya Palestina imelaani vikali hatua ya utawala ghasibu wa Israel ya kubomoa makasri ya utawala wa Banu Umayya yaliyopo katika eneo la kusini mwa Msikiti wa al-Aqsa.
Kwa mujibu wa tovuti ya Palestineinfo, utawala huo unabomoa majengo hayo ya historia ya Kiislamu kwa shabaha ya kupanua ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi katika maeneo hayo.
Kamati ya Quds iliyopo chini ya wizara iliyotajwa inasema kwamba utawala wa Kizayuni unayabomoa makasri hayo kwa lengo la kujenga bustani ya Mayahudi na pia njia ya chini kwa chini itakayoliunganisha eneo hilo na eneo jingine la Silwan.
Kamati hiyo pia imelaani kitendo cha hivi karibuni cha utawala huo cha kuharibu nyumba mbili katika mtaa wa Beit Huneina kaskazini mwa Quds kwa kisingizio kwamba zimejengwa hapo kinyume cha sheria.
Wizara ya Masuala ya Kidini ya Palestina pia imelaani katika taarifa hiyo mateso yanayofanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina na kuongeza kuwa mateso hayo si mapya na kwamba yanafanyika katika kudumisha mwenendo wa jinai za utawala huo dhidi ya Wapalestina wakazi wa Quds Takatifu. 758690
captcha