Wakizungumza kwa njia ya simu, Marais Asif Ali Zardari wa Pakistan na Abdallah Gul wa Uturuki wamechunguza dharau iliyofanywa hivi karibuni dhidi ya kitabu kitakatifu cha Qur'ani katika mojawapo ya makanisa ya Jimbo la Florida huko Marekani.
Marais wawili hao wamesisitiza katika mazungumzo yao juu ya ulazima wa kufuatilia jambo hilo katika ngazi za kimataifa ili kuzuia kukaririwa tena kwa hatua kama hizo za kuvuka mipaka. Rais Zardari ametaka kuimarishwa kwa umoja wa umma wa Kiislamu ili kukabiliana na hatua hizo za kijinai. Amewataka Waislamu wafuatilie kimataifa hatua ya Terry Jones kasisi mwenye misimami ya kupindukia mipaka wa kanisa la jimbo la Florida, ya kuchoma Qur'ani na kuchukua stratejia inayofaa ili kuzuia kukaririwa kwa kitendo hicho kinachokosea heshima thamani na matukufu ya Kiislamu. Mwishoni mwa mazungumzo hayo ya simu Rais Zardari amesisitiza kuwa kitendo hicho cha dharau bila shaka kitaongeza tu hasira ya Waislamu dhidi ya maadui wao duniani. 766677