Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, aliyasema hayo Jumatatu jioni, Machi 28, 2011, aliponana na wahandisi, mafundi na wafanyakazi wa sekta ya mafuta katika eneo la Pars Kusini pamoja na mjumuiko wa familia tukufu za mashahidi wa eneo hilo na huku akiashiria juu ya suala la kupewa mwaka huu wa 1390 (Hjiria Shamsia) jina la mwaka wa "Jihadi ya Kiuchumi" amesema, taifa la Iran limesimama imara kwa muda wa miaka 32 katika kupambana na mabeberu wa dunia na kwamba jihadi na mapambano hayo yataendelea kwa sura tata zaidi, ya kina zaidi na nyeti zaidi katika uga wa kiuchumi.
Aidha ameutaja welewa na kushikamana taifa la Iran pamoja na utamaduni wa jihadi kuwa ni katika nembo za maendeleo mtawalia ya Iran katika nyuga mbali za ulinzi, sayansi na siasa na kuongeza kuwa, tofauti iliyopo baina ya "jihadi ya kiuchumi" na "juhudi za kiuchumi" ni kwamba, maana halisi ya "jihadi ya kiuchumi" inaonekana kwa kuingia katika medani ikizingatiwa kuwa kuna maadui wanapinga maendeleo ya taifa la Iran na kwa hakika jambo hilo huwafanya wananchi wa matabaka yote na viongozi wote nchini iwabidi washiriki vilivyo kwenye mapambano hayo.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria juu ya njama za mabeberu wa dunia za kujaribu kukwamisha maendeleo ya taifa la Iran na kuongeza kuwa, kazi kubwa iliyofanyika katika eneo la Pars Kusini ni aina moja wapo ya jihadi ya kiuchumi katika njia ya Mwenyezi Mungu kwani imefanyika kwa nia ya kupigania utukufu wa Uislamu na neno la haki na vile vile kwa ajili ya kuliletea maendeleo na kuliongezea heshima taifa la Iran.
Vile vile amewashukuru wataalamu, wafanyakazi na wahusika wote katika miradi mbali mbali za maendeleo kwenye medani ya Pars Kusini na kuongeza kuwa, kazi za kijihadi za namna hiyo zinaweza kuliletea taifa ustawi wa kudumu kupitia uzalishaji wa elimu za kimsingi.
Amesema maendeleo waliyopata wananchi wa Iran katika kipindi cha miaka 32 iliyopita ni katika ufanikishaji wa ahadi za Mwenyezi Mungu zilizo lazima kutimia yaani ahadi za kushinda jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu. Ameongeza kuwa, wananchi na viongozi katika sekta mbali mbali nchini wanapaswa kupigana jihadi ya kiuchumi katika njia ya Mwenyezi Mungu kwa nguvu zao zote na Mwenyezi Mungu atatia baraka Zake katika mapambano yao hayo Inshaallah.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameyataja masuala kama kutegemea vipaji vya kizazi cha vijana na uwezo wa ndani, kuwa na hisia za kutowahitajia wageni na kujiegemeza kwenye chemchemu inayochemka kwa nguvu ya irada thabiti ya taifa kuwa ndiyo njia ya utatuzi wa matatizo yote na huku akitoa mifano ya wazi ya jihadi na mapambano ya kiuchumi ameongeza kuwa, matumizi sahihi na kujiepusha na israfu na ufujaji, kudumisha utamaduni wa kupenda kuchapa kazi na kufanya juhudi kilillahi na kuwafundisha vijana utamaduni huo muhimu, kupiga hatua kuelekea kwenye maendeleo na uadilifu na kufanya juhudi bila kuchoka kwa ajili ya kuwatatulia wananchi matatizo yao na kuwakidhia mahitaji yao ni mambo ambao yanapaswa kuwa sehemu ya majimui ya jihadi ya wananchi na viongozi wote katika mwaka huu wa "Jihadi ya Kiuchumi."
Amesema kwamba, kuwa na mshikamano, kupendana, kusaidiana, kushirikiana na kuenea hisia za udugu na kufanya jitihada za pamoja ndiyo siri ambayo siku zote inaliwezesha taifa la Iran kuwashinda maadui wa Uislamu na maadui wa Iran na kuongeza kuwa, mchakato wa kuongezeka heshima na adhama ya taifa la Iran utaendelea.
Ayatullah Udhma Khamenei pia ameelezea kufurahishwa kwake na mambo aliyoyaona wakati alipotembelea sehemu tofauti za medani ya Pars Kusini na kusisitiza juu ya udharura wa kufanyika utafiti wa kina na wa kisayansi katika masuala ya mafuata na gesi. Amesema kazi kubwa sana alizoziona kwenye eneo hilo zinaonesha kuwa rasilimali kubwa ya taifa la Iran ni kuwa na hisia za kujiamini na kuhisi linaweza kufanya linalopenda kufanya na kwamba taifa linapokuwa na hisia hizo huweza kufanya kazi yoyote linayoamua.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aidha amesema, mafuta na gesi ni mali za umma na ni mali ya kila mtu nchini na wakati huo huo ameongeza kuwa, nguvu kazi yenye vipaji na yenye uwezo na hamu ya kufanya kazi ndiyo rasilimali kubwa na ya asili ya nchi kwa ajili ya kufika kwenye vilele vya juu ya maendeleo na utukufu.
Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, historia ya wananchi wa mkoa wa Bushehr (kusini mwa Iran) imejaa jihadi katika njia ya uhuru na heshima ya taifa. Ameongeza kwa kusema: "Kwa bahati nzuri anga jumla ya nchi ni anga ya kufanya kazi, ni anga ya kuongeza juhudi na kupendana na kwamba taifa la Iran haliwezi kusahau jihadi na kujitolea kukubwa kulikofanywa na "mashahidi, majeruhi wa vita na watu wanaojitolea katika njia ya Mwenyezi Mungu" ambao wamelipa taifa fursa bora na ya kihistoria ya kujiletea maendeleo."
Mwanzoni mwa mkutano huo, Ayatullah Safayi Bushehri, Mwakilishi wa Fakihi Mtawala katika mkoa wa Bushehr ambaye pia ni Imam wa Ijumaa wa mkoa huo amemkaribisha Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu mkoani humo na kusema kwamba mkoa wa Bushehr ni moja ya maeneo muhimu ya kufanyia jihadi ya kiuchumi na kwamba wananchi wa mkoa huo watafanikiwa kwenye medani hiyo kama walivyofanikiwa katika medani nyinginezo za jihadi na mapambano kwa kutegemea umoja, juhudi na kuchukulia mambo kwa uzito wa hali ya juu.
Naye Bw. Masoud Mir Kazemi, Waziri wa Mafuta wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa mara nyingine amewawakilisha wafanyakazi wa sekta ya mafuta kumkaribisha Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na kuongeza kuwa, juhudi zote za wafanyakazi wa sekta ya mafuta nchini zinalenga kwenye kufanikisha malengo makuu ya ustawi na uadilifu.
766791