Mashia hao pia hawana haki ya kuchapisha vitabu vya kidini na vile vinavyoingizwa nchini humo kutoka nchi jirani hunaswa na kuharibiwa na maafisa wa utawala wa nchi hiyo. Mashia wanalalamikia vikali jambo hilo na kusema kuwa hawapewi hata haki ya kutayarisha vipindi vya kawaida kabisa vya kidini vikiwemo vile vinavyohusiana na mwezi mtukufu wa Ramadhani. Magazeti ya utawala wa Kiwahhabi wa Saudi Arabia pia hayaruhusiwi kuchapisha wala kuakisi shughuli na mambo yanayowahusu Mashia wa nchi hiyo. 766999