IQNA

Semina ya ‘Vyombo vya habari, na maadili ya kibinaadamu’ kufanyika Malaysia

14:05 - April 04, 2011
Habari ID: 2100432
Semina yenye anuani ya ‘Vyombo vya habari, na maadili ya kibinaadamu’ kitafanyika mjini Kuala Lumpur nchini Malaysia Aprili sita katika Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Kiislamu.
Mkutano huo umeandaliwa kwa ushirikiano na Kituo cha Mazungumzo cha Uturuki na Malaysia, Mashirika ya Karangkraf na Jarida la Fountain. Lengo la semina hiyo limetajwa kuwa ni kuimarisha ushirikiano wa vyombo vya habari ili kutangaza thamani za mataifa na kudumisha maadili mema katika jamii ya kisasa.
Abdul Jalil Ali Mkurugenzi wa Kituo cha Habari cha Karangkraf, Nasal Mohammad wa Kanali ya Televisheni ya Al Hijrah, Hakan Yesilova Mhariri Mkuu wa Jarida la Fountain na Kristof Martin Kovoski wa Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Kiislamu watahutubu katika duru ya kwanza ya semina hiyo.
Duru ya pili ya kikao hicho itahutubiwa na John Paul mtaalamu wa Historia ya Ukristo Marekani Kaskazini, Profesa Ahmad Murad Merican wa Kitivo cha Menejmenti na Elimu za Jamii katika Chuo Kikuu cha Petronas cha Malaysia na Profesa Radhi al Mubarak mkuu wa idara ya elimu za saikolojia ya elimu katika Chuo Kikuu cha Iowa Kaskazini nchini Marekani.
768119
captcha