Kwa mara nyingine tena wananchi wa Afghanistan wamefanya maandamano makubwa ya kulaani kitendo cha kuchomwa moto Qur'ani Tukufu nchini Marekani. Mandamano hayo yalifanyika jana Jumanne katika mji mkuu wa nchi hiyo, Kabul.
Kwa mujibu wa tovuti ya Dawn, mamia ya waandamanaji walikusanyika mbele ya Chuo Kikuu cha Kabul na kupiga nara za 'mauti kwa Marekani' na 'wanaokosea heshima Qur'ani wanapaswa kushtakiwa.' Maandamano hayo yalianzia mbele ya chuo kikuu hicho na polisi kuchukua hatua ya kufunga njia zote zinazoelekea katika chuo hicho. Watu watano wameuawa katika ghasia na polisi na wengine wengi kujeruhiwa katika maandamano hayo ya siku mbili yaliyogeuka na kuwa ya ghasia huko katika mji wa Kandahar ulioko kusini mwa Afghanistan. Maandamano mengine makubwa kama hayo yamefanyika katika mji wa kaskazini wa Mazar Shariff kulalamikia kitendo cha kasisi mwovu Terry Jones wa jimbo la Florida nchini Marekani cha kuchoma moto Qur'ani Tukufu. 769468