IQNA

Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran asema Marekani inawapa himaya madikteta

18:01 - April 09, 2011
Habari ID: 2102279
Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa mjini Tehran amesema kuwa, harakati za hivi sasa za mapinduzi katika nchi za Kiislamu ni dalili ya wa wazi kwamba, Waislamu kamwe hawaukubali wala kuuridhia udikteka.
Hujjatul Islam wa Muslimin Sheikh Kazem Sidiq amesema hayo mbele ya hadhara ya waumini waliohudhuria ibada ya kisiasa na kimaanawi ya Sala ya Ijumaa mjini Tehran na kusisitiza kwamba, ikulu ya Marekani White House ndio muungaji mkono mkubwa wa tawala za kidikteta katika Mashariki ya Kati. Sheikh Kazem Sidiq ameashiria kitendo cha kishenzi cha hivi karibuni cha kasisi Terry Jones wa Florida Marekani na wenzake cha kuchoma moto nakala za Qur'ani Tukufu na kusema kuwa, kimya cha viongozi wa White House kinaonyesha woga walionao wa kuenea matukufu ya Kiislamu ulimwenguni. Aidha khatibu wa Sala ya Ijumaa hapa Tehran ameashiria maendeleo makubwa ya Iran katika uga wa kielimu na kusisitiza kwamba, serikali ya Tehran na wananchi shupavu wa Iran wameazimia kwa dhati kustafidi na teknolojia ya kisasa ya nishati ya nyuklia na kwamba wanatambua kwamba, hii ni haki yao kisheria; hivyo hakuna kulegeza kamba katika hili.
770608
captcha