Mashindano hayo yameandaliwa na Kamati ya ad-Dhakiraat inayofungamana na Jumuiya ya Taaluma ya Qur'ani Tukufu ya mji wa Umm al-Humaam. Kamati hiyo imetangaza kwamba uandikishaji wa majina ya washiriki wa mashindano hayo ilianza tarehe 5 Aprili. Mashindano hayo yatafanyika katika hatua tofauti za hifdhi ya Qur'ani nzima, juzuu 10 tokea Sura ya Yunus hadi Qiswas, Juzuu 5 tokea Sura al-Israa hadi Qiswas na hifdhi ya juzu za 29 na 30 za kitabu hicho kitakatifu. Udhibiti kamili wa tajwidi katika usomaji Qur'ani ni moja ya masharti muhimu ya kushiriki katika mashindano hayo, na tarehe ya mwisho ya kujiandikisha ni hapo tarehe 19 Septemba. 770145