Kwa mujibu wa gazeti la al-Qabas linalochapishwa nchini Kuwait, mabalozi hao wamelaani vikali kitendo hicho cha Kasisi Terry Jones na kuitaka Vatican ichukue msimamo wa wazi kuhusiana na dharau hiyo dhidi ya matukufu ya Kiislamu. Wamesema kuwa kitendo hicho kiovu kinakwenda kinyume na thamani za ustaarabu wa mwanadamu na kutaka Vatican ikilaani kwa maneno makali. Mabalozi hao wa nchi za Kiislamu wamebainisha wazi wasiwasi wao kuhusiana na matokeo mabaya ya kitendo hicho cha dharau ulimwenguni. Tunakumbusha hapa kuwa Kasisi Terry Jones tarehe 20 Machi alitekeleza tishio lake alilotoa huko nyuma la kuchoma moto Qur'ani Tukufu na hivyo kuamsha hasira ya ulimwengu wa Kiislamu dhidi ya kasisi huyo na maadui wengine wa Uislamu wanaokosea heshima matukufu ya Kiislamu. 770553