Jumuiya ya Maulama wa al-Azhar imetoa taarifa ikitangaza kwamba dharau iliyofanywa na Muhammad Ridha Muharram, mhadhiri katika Chuo cha Uhandisi cha al-Azhar, dhidi ya Mtume Muhammad (saw) ilifanyika kwa uungaji mkono wa hayati Muhammad Tantawi, sheikh wa zamani wa al-Azhar kwa lengo la kuboresha uhusiano na utawala haramu wa Israel.
Wanazuoni wa al-Azhar wanamtuhumu Murram kwamba alimkosea heshima Mtume Mtukufu katika kipindi cha uongozi wa Tantawi kwa kumtaja mtukufu huyo kupitia televisheni za satalaiti kwamba alikuwa haamini mafundisho ya kidini na kwamba alikuwa msekula. Wanazuoni hao pia wamezilaumu televisheni zinazomwalika mhadhiri huyo kuzungumza katika vipindi vyao kwa kusema kuwa kufanya hivyo ni kushajiisha na kueneza duniani fikra za kisekula zinazopinga dini. Taarifa ya wanazuoni hao wa al-Azhar imeashiria safari za mara kwa mara za Muharram huko Israel na kusema kwamba safari hizo zilifanyika kwa uungaji mkono wa Ahmad Omar Hashim, mkuu wa wakati huo wa Chuo cha al-Azhar na Muhammad Tantawi. 772275