IQNA

Kamisheni ya Kiislamu-Kikristo ya Palestina yaonya juu ya ujenzi wa vitongoji vya Mayahudi huko Quds

12:53 - April 14, 2011
Habari ID: 2105676
Kamisheni ya Kiislamu na Kikristo ya Palestina inayotetea Quds na maeneo mengine matakatifu huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Israel, imeonya juu ya hatari ya njama za kuenezwa ujenzi wa vitongoji vya Mayahudi katika maeneo hayo na hasa Quds, njama zinazotekelezwa na utawala huo haramu.
Akizungumzia suala hilo, Hassan Khatir, Katibu Mkuu wa kamisheni hiyo amedokeza kwamba mpango wa kujengwa vitongoji vya Mayahudi katika mji wa kale wa Quds unatekelezwa kwa kasi kubwa na utawala huo wa Kizayuni. Amesema mpango huo unatekelezwa kwa kubomoa nyumba na maeneo ya Kiislamu na kufuta kabisa majina ya mitaa ya Kiislamu na Kiarabu na kuibadilisha na majina ya Kiyahudi. Amesema mpango huo umekuwa ukitekelezwa na utawala huo kwa miaka 10 sasa kwa kisingizio cha kukarabati maeneo ya kale na kihistoria. Hassan Khatir ameendelea kusema kwamba Kamati ya Kiislamu na Kikristo ya Kutetea Quds na Maeneo Matakatifu ya Palestina imekuwa ikipiga picha na kuorodhesha maeneo hayo yote, ambapo imeazimia kuwatumia viongozi wa nchi za Kiislamu. Khatir amekosoa vikali radiamali dhaifu kutoka kwa nchi za Kiislamu na Kiarabu kuhusiana na suala hilo. 773877
captcha