Waislamu hao wameelezea wasiwasi wao mkubwa kuhusiana na mauaji yanayoendelea kufanywa na askari wa Saudia dhidi ya Waislamu wenzao huko Bahran. Maandamano hayo ambayo pia yaliyajumuisha makundi mengi ya wateteaji wa haki za binadamu yamekemea vikali uingiliaji kijeshi wa Saudia katika nchi hiyo jirani na kuitaka iondoe haraka askari wake katika ardhi ya nchi hiyo. Waandamanaji wamesema uingiliaji wa kijeshi wa Saudia ni hatua ya kigaidi na kuutaka pia utawala wa Baharin uwaachilie huru mara moja wafungwa wote wa kisiasa wakiwemo wanawake na watoto unaowashikilia na kuwatesa kwenye jela. Wametaka tawala mbili hizo za Bahrain na Saudia kuacha mara moja kumwaga damu za Waislamu na kubomoa maeneo yao ya ibada ikiwemo misikiti pamoja na makaburi ya mawalii wa Mwenyezi Mungu. 775433