IQNA

Uungaji mkono wa Waislamu wa Karachi kwa watu wa Bahrain

12:00 - April 19, 2011
Habari ID: 2108309
Siku ya Jumapili Waislamu wa Karachi nchini Pakistan walifanya maandamano makubwa ya kulaani kitendo cha kuchomwa Qur'ani, kubomolewa misikiti na vilevile kuwaunga mkono Waislamu wenzao wa Bahrain wanaoendelea kukandamizwa na utawala dhalimu wa ukoo wa Khalifa.
Maandamano hayo yameandaliwa na Jumuiya ya Wanachuo wa Imamia ISO na Majlisi ya Umoja wa Waislamu MWM. Waandamanaji wamelaani vikali mauaji ya kiholela yanayofanywa dhidi ya waandamanaji wanaopigania haki zao kwa njia za amani katika nchi za Bahrain, Libya na Yemen na wakati huohuo kukemea uchochezi unaofanywa na Marekani na utawala haramu wa Israel dhidi ya Waislamu nchini Bahrain. Wamezitaka nchi za Saudi Arabia, Imarati, Kuwait na nchi nyinginezo za Ghuba ya Uajemi kujiepusha kutuma askari jeshi wao huko Bahrain kwa ajili ya kutekeleza ukandamiza na mauaji dhidi ya watu wasio na hatia wa nchi hiyo. 776463
captcha