IQNA

Nafasi ya Misikiti katika Jihadi ya Kiuchumi

18:31 - April 20, 2011
Habari ID: 2109301
Misikiti inaweza kutumika kama eneo bora zaidi la kubainisha 'Jihadi ya Kiuchumi' kwa lengo la kutambua njia za kiutamaduni za kufanikisha jihadi hiyo.
Hayo yamesemwa na Naibu Mwenyekiti wa Kamati ya Sera za Kigeni na Usalama wa Kitaifa katika Bunge la Iran (Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu) Hujjatul Islam Hussein Ibrahimi ambaye amesema 'Jihadi' ni neno takatifu katika msamiati wa Kiislamu.
Amesema kwa mujibu wa Qurani Tukufu, Jihadi inamaanisha kufanya juhudi maalumu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Amesema neno hilo linaweza pia kumaanisha kujitolea kwa malengo ya kidini.
Itakumbukwa kuwa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyed Ali Khamenei aliutangaza mwaka mpya wa Kiirani 1390 ulioanza Machi 21 kuwa mwaka wa 'Jihadi ya Kiuchumi'.
777548


captcha