IQNA

Hija: Msimu wa umoja na mwamko wa kisiasa kwa Umma wa Kiislamu

18:11 - May 29, 2026
Habari ID: 3482298
IQNA – Mwandishi na mwandishi wa habari kutoka Morocco amesisitiza kuwa Hija ni fursa ya kuimarisha kuishi kwa pamoja, kukubali tamaduni za wengine, na kufunguka kwa desturi na mila za mataifa mbalimbali.

Akizungumza katika mahojiano na IQNA, Hayat Lalab alisema Hija huchukuliwa kuwa ni msimu wa umoja mkubwa wa kijamii na kisiasa, na “mwamko” kwa Umma wa Kiislamu, wakati zaidi ya mahujaji milioni 1.7 wakiendelea kutekeleza ibada za mwisho za Hija ya 1447  (2026) katika mji mtukufu wa Makkah.

Hija ni miongoni mwa nguzo na ibada kuu za Uislamu; ni faradhi inayojumuisha taratibu na amali mbalimbali zinazotekelezwa kupitia safari ya kwenda Makkah katika Hijaz. Huko, Mwislamu hutekeleza ibada zenye sura ya kiroho, lakini pia zikiwa na vipengele vya kijamii, kiuchumi na kisiasa. Hija pia ndio mkusanyiko mkubwa zaidi wa Waislamu, ambapo makundi kutoka madhehebu mbalimbali hukusanyika Makkah katika msimu maalumu.

Kwa lengo la kuonesha nafasi ya Hija katika kukuribisha madhehebu za Kiislamu, kuimarisha umoja wa Umma, falsafa ya faradhi hii, pamoja na athari zake kijamii na kimataifa, Shirika la Habari la IQNA limefanya mahojiano na Hayat Lalab kama ifuatavyo:

 

IQNA: Unaipimaje nafasi ya Hija katika kukuribisha madhehebu za Kiislamu na kuimarisha umoja wa Umma wa Kiislamu?

Lalab: Hija ina vipengele vingi, ya kidini, kisiasa, kiuchumi na kitamaduni, na ni msimu ambao Waislamu wa lugha, rangi na madhehebu mbalimbali hukutana pamoja. Uislamu unatufundisha kuwa Hija ni mkutano wa kidini unaozifanya nyoyo za undugu wa Kiislamu zifungamane zaidi, bila kujali tofauti za lugha au madhehebu; mahali ambapo tofauti hupotea na Waislamu “huyeyuka” pamoja katika ibada na tauhidi. Imam Khomeini (RA) pia alisisitiza kuwa Hija ni msimu wa umoja na ufufuo mkubwa wa kisiasa na kijamii kwa Umma wa Kiislamu.

 

IQNA: Falsafa ya Hija ni ipi? Kwa nini Waislamu hukusanyika kutoka kila pembe ya dunia, na safari hii huathirije roho za mahujaji?

Lalab: Waislamu hukusanyika kutoka sehemu mbalimbali za dunia kutekeleza wajibu ambao Mwenyezi Mungu amewafaradhisha wote. Hija ni safari kuu yenye maana nyingi, na ni kongamano la kila mwaka ambapo Waislamu hukutana katika ardhi tukufu.

Kwa upande wa athari yake katika roho za mahujaji, wanaporejea makwao huwa na uhusiano imara zaidi na Mwenyezi Mungu kuliko hapo awali. Ibada za Hija huilea nafsi na kuleta utulivu katika roho za mahujaji. Hija pia hutufundisha sifa kama unyenyekevu, hisia ya kuwajibika, na mambo mengine ambayo mhujaji huyajifunza katika safari yake ya kuelekea Nyumba Tukufu.

IQNA: Maana ya Wuquf (kusimama/kukaa) Arafat na Masha’ar al-Haram ni ipi? Nini umuhimu wa kiroho wa sehemu hizi mbili?

Lalab: Wuquf Arafat ni miongoni mwa nguzo za Hija, na hufanywa kwa nia ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu na kwa unyenyekevu kamili mbele Yake. Siku ya Arafah ina maana nyingi nisizoweza kuzitaja zote, lakini nitagusia baadhi: Mandhari ya Wuquf Arafat hutukumbusha watu watakaposimama mbele ya Mwenyezi Mungu Siku ya Kiyama. Pia siku hii iliteremshwa aya ya kukamilishwa kwa dini (ambayo ni wilaya ya Imam Ali (AS)). Jambo kuu zaidi Arafat ni kuwa Imam Zaman (AJ) yupo miongoni mwa mahujaji na huwafunika kwa baraka za uwepo wake.

Kwa upande mwingine, Wuquf Arafat ni kukiri dhambi na upungufu mbele ya Mwenyezi Mungu, na siku ya Arafah huhesabiwa kuwa ni siku iliyojaa baraka na fadhila za Kiungu kwa mahujaji.

IQNA: Kutupia mawe Jamarat kunaashiria nini? Kwa nini mahujaji hutupia mawe nguzo maalumu, na tukio gani katika maisha ya Nabii Ibrahim (A.S.) tendo hili hutukumbusha?

Lalab: Kwa mujibu wa riwaya kutoka kwa Imam Ali (A.S.), sababu ya kutupia mawe inarejea katika kisa cha Nabii Ibrahim (AS). Wakati Malaika Jibril alipomwonyesha alama/mafundo ya ibada, Iblis (Shetani) alijitokeza mbele yake, ndipo Jibril akamwamuru amtupie mawe saba.

Kutokana na kutupia mawe Shetani, tunaelewa kuwa tendo hili ni alama ya kusimama imara dhidi ya uovu—uovu unaojitokeza katika sura ya Shetani, wafuasi wake, na kila anayewaita watu kwenye njia isiyo ya Mwenyezi Mungu.

IQNA: Falsafa ya kuchinja katika Idd al-Adha na kugawa kwa wahitaji ni ipi?

Lalab: Kuchinja wakati wa Hija ni miongoni mwa amali za wajibu za Hija; mnyama wa kuchinja hupaswa kuwa miongoni mwa mifugo kama kondoo, ng’ombe au ngamia.

Kuchinja siku ya kumi ya Dhul-Hijjah, kwa upande mmoja, huleta upanuzi wa riziki kwa familia; na kwa upande mwingine, huonesha kuwajali wahitaji na masikini wasiokuwa na uwezo. Nao ni wengi, hasa ukizingatia idadi kubwa ya mayatima, familia za mashahidi, na majeruhi. Kwa hivyo, ni lazima tuwatazame kwa jicho la huruma na kuufanya msimu wa Idd kuwa furaha kwa masikini, mayatima waliopoteza baba wakiwa watoto, na wanawake waliopoteza waume bila mlinzi wala riziki. Kwa hiyo tunapaswa kuielewa dhana ya kuchinja kwa mtazamo wa kina na wa ujumla zaidi.

3497635

Habari zinazohusiana
captcha