IQNA

Mwamko wa Kiislamu katika eneo hauwezi kuzimwa na yeyote

11:10 - April 23, 2011
Habari ID: 2109912
Khatibu wa muda wa Sala ya Ijumaa hapa mjini Tehran Ayatullah Mohammad Emami Kashani amesema leo kuwa muamko wa Kiislamu unaoshuhudiwa katika eneo la Mashariki hivi sasa hauwezi kuzimwa na mtu yeyote.
Akihutubia umati mkubwa wa Waislamu wakati wa Sala ya Ijumaa kwenye uwanja wa Chuo Kikuu cha Tehran, Ayatullah Kashani amelikosoa Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi kwa misimamo yake ya kindumakuwili kuhusu mwamko unaoshuhudiwa katika eneo hili. Amesema kwa upande mmoja baraza hilo limetangaza kuwaunga mkono wananchi wa Syria na Libya na kwa upande mwingine limefumbia macho jinai wanazofanyiwa wananchi wa Bahrain na Yemen wanaoandamana kupinga tawala za kiimla katika nchi hizo. Amesisitiza kuwa Mashariki ya Kati mpya inaelekea kuzaliwa na hakuna mtu yeyote anayeweza kuzima ari ya wananchi wa eneo hili ya kutaka usawa na uadilifu kwenye safu ya uongozi.
778672
captcha