IQNA

Warsha ya tarjumi ya Qur'ani kufanyika Tehran

21:26 - April 27, 2011
Habari ID: 2113374
Waziri wa Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu wa Iran amesema warsha ya tarjumi ya Qur'ani itafanyika katika Maonyesho ya 24 ya Vitabu ya Tehran.
Sayyid Mohammad Husseini amesema maonyesho hayo ndio tukio kubwa zaidi la kiutamaduni nchini Iran.
Ameongeza kuwa wachapishaji zaidi ya 2000 wa Iran watashiriki katika maonyesho hayo ambapo watawasilisha anwani 208,000 za vitabu katika kitengo cha kitaifa.
Amesema kwa kuzingatia kuwa maonyesho ya mwaka huu yanasadifiana na siku za kukumbuka kuuawa shahidi Bintiye Mtume SAW, kutakuwa na kitengo maalumu cha maisha ya Bibi Fatima Zahra AS.
Maonyesho ya 24 ya Kimataifa ya Vitabu ya Tehran yatafanyika Mei 4-14 katika Ukumbi wa Sala wa Imam Khomeini.
781478
captcha