Kwa mujibu wa tovuti ya Today.gm, wazazi walio na hamu ya kuwawezesha watoto wao wahifadhi Qur'ani wanaweza sasa kuwasajili watoto wao katika kituo hicho.
Mbali na kutoa mafunzo ya hifdhi ya Qur'ani kituo hicho pia kitakuwa kikitoa masomo ya msingi ya Uislamu na thamani za kiakhlaqi na kimaadili. Wasimamizi wa kituo hicho wanasema kuwa kuasisiwa kwake kunaonyesha jinsi watu wa Gambia wanavyozingatia mafunzo ya Qur'ani.
Akizungumzia suala hilo, Bafudi Fato, naibu mkuu wa Taasisi ya Vijana wa Kiislamu wa Kerewan amesema kwamba kuongezeka kwa idadi ya walimu na wataalamu wa masuala ya mafundisho ya Qur'ani katika mji huo ni moja ya sababu zilizopelekea kuasisiwa kwa kituo hicho cha hifdhi ya Qur'ani. Ametaka taasisi na mashirika mengine yanayojishughulisha na masuala ya Qur'ani katika mji huo kushirikiana na kituo hicho ili kufanikisha malengo yake.
Amesema kabla ya kufunguliwa kituo hicho, wazazi walikuwa wakiwapeleka watoto wao katika vituo vya mbali ili kupata masomo ya Qur'ani lakini kwamba hivi sasa wazazi hao watapunguziwa mzigo wao kwa sababu watoto wao sasa watakuwa wakipata masomo hayo katika mji wao wenyewe. 782342